Quantcast
Channel: SUAMEDIA | Sokoine University of Agriculture TV and Radio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 10

SUA yasema hakuna haja ya kuogopa chanjo ya UVIKO 19

$
0
0

Na Gladness Mphuru

Morogoro

Makamu Mkuu  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda, amezindua chanjo ya COVID 19 aina ya Janssen dozi 500 chuoni hapo, ikiwa ni muendelezo na utekelezaji wa kampeni ya Taifa ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Makamu Mkuu  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda katika picha ya kushoto akizungumza na wanajumuiya wa SUA hawapo pichani na picha ya kulia akipata chanjo ya UVIKO 19

Prof. Chibunda amefanya uzinduzi huo leo, Augosti 4, 2021, akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo, akiwemo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala, Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Muhairwa na Daktari mkazi wa Hospitali za SUA Dkt. Omary Kasuwi.

Prof. Chibunda amesema kutokana na Jamii inayoizunguka taasisi hiyo, ikiwemo Jumuiya ya Wanafunzi na Wafanyakazi kufikia takribani watu elfu 20 ndio sababu kubwa ambayo imepelekea kufanyika kwa juhudi za kutuma maombi mkoani ili jumuiya hiyo iwe salama.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) Prof. Maulid Mwatawala kushoto na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mwairwa kulia wakichanja UVIKO 19 

“Tumefanya juhudi kubwa kwa watu wa mkoani angalau na sisi watuhusishe kama kituo, sababu kubwa ya kupeleka maombi hayo ilikuwa kwanza kuna watu wengi tunaoishi pamoja, na katika Manispaa hii ya Morogoro hakuna taasisi yenye watu wengi kama SUA” amesema Chibunda

Prof. Chibunda amesema jambo jingine lililopelekea kuomba kupata chanjo hiyo ni kuwa pamoja na kutaka kuchanja katika maeneo yaliyopangwa lakini ilionekana watu kutoka SUA katika cha sabasaba walikuwa ni wengi na hiyo ilionyesha jinsi taasisi hiyo ya kisayansi ilivyoamua kupata chanjo hiyo ya UVICO 19.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mwairwa, amewaasa wanajumuiya wa SUA na watanzania kujitokeza na kuacha ubishi juu ya chanjo sanjari na kuepuka upotoshaji wa chanjo hasa kwenye mitandao ya kijamii, bali wasikilize maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya.

Awali akizungumza katika zoezi hilo la chanjo Daktari Mkazi wa Hospitali za SUA Dkt. Omary Kasuwi, amesema wimbi la kwanza la virusi vya CORONA vilivyoanza mnamo mwaka 2019 na 2020 ilikuwa kipindi kigumu kwa Hospitali ya SUA, kwani walipokea takribani watu 2000 wenye maambukizi na watu 5 kati yao walifariki.

Daktari Mkazi wa Hospitali za SUA Dkt. Omary Kasuwi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Magonjwa ya ndani ya Mwili kushoto akipata chanja ya UVIKO 19 na kulia ni wauguzi kutoka SUA wakiwa tayari kwa zoezi la chanjo

“Cha msingi tunaweza tukajifunza nini kimetokea duniani na hasa ulaya, vifo vilivyotokea 2019 na 2020 na idadi ya vifo katika kipindi cha mwezi januari kwa mwaka 2021 unaweza kuona kulikuwa na ongezeko kidogo nah ii inaonyesha kirusi hiki cha ‘Delta’ ni hatari sana” amesema Kasuwi


The post SUA yasema hakuna haja ya kuogopa chanjo ya UVIKO 19 appeared first on SUAMEDIA | Sokoine University of Agriculture TV and Radio.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 10

Latest Images

Trending Articles





Latest Images